Monday, August 13, 2018

Nyumbani Kumenoga

Mtandao wa simu za mkononi wa TTCL Corporation, sasa unapatikana nchi nzima, mikoa yote.
Simu zote janja na za kawaida (GSM) au vitochi zinakamata mtandao.
Ili kujiunga na kifurushi cha BoomPack, unatakiwa kubofya *148*30*35 alama ya reli.

Monday, April 21, 2014

Kuitambulisha Bajaj RE 4S Mpya

Jukwaa linalotembea la Experiential Marketing, likitoa elimu na burudani maeneo ya Mbagala jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya sifa muhimu za Bajaj RE 4 S ni hizi zifuatazo:
1. Mfumo wa injini wenye plagi mbili pacha.
2. Injini ina pistoni moja na valvu mbili.
3. Mfumo wa injini wenye mapigo manne kwenye chemba ya aluminiamu.
4. Ina kipoza injini chenye mfumo wa hewa na oili.
5. Chasisi imara zaidi.
6. Kebini imeongezewa nafasi zaidi.
7. Ina sehemu ya kuchaji simu.
8. Ina kihifadhi cha chupa ya maji.
9. Kizuia matope kimetengenezwa kwa chuma.
10. Nafasi katika uvungu ni sentimeta ishirini.
Sifa hizi na nyinginezo nyingi zinakupa ubora na thamani ya pesa yako.

Thursday, February 13, 2014

Siku ya Radio Duniani






Leo Tarehe 13 mwezi wa Februari 2014, ni Siku ya Radio Duniani. 

Mwaka 2011 UNESCO ilipitisha azimio la kuifanya tarehe 13, Februari kuwa Siku ya Radio Duniani, ili kutoa wito kwa watu kuzingatia umuhimu wa Radio, kuhamasisha nchi mbalimbali kuendeleza upashanaji wa habari kwa njia ya radio na kuimarisha ujenzi wa mtandao na ushirikiano wa kimataifa kati ya vituo vya radio.

 Mkuu wa idara ya taarifa kwa umma na mahusiano na nje wa UNESCO Neil Ford ananukuliwa akisema:
"Huu ni mwaka wa tatu wa maadhimisho ya Siku ya Radio Duniani, na mwaka huu kauli mbiu ni usawa wa jinsia katika radio. Tunatarajia kuwa vituo vya radio vya nchi mbalimbali vinaweza kufikiri na kujadili kwa makini mada hiyo. Mwaka huu, vituo vinane vya radio kutoka sehemu mbalimbali duniani kama:  Radio China Kimataifa, Radio ya Kimataifa ya Ufaransa, Radio ya Hispania, Radio ya Lebanon na nyingine pia vitafanya matangazo ya moja kwa moja katika makao makuu ya UNESCO, na hii itakuwa ni kama sikukuu ya radio”.

"Ingawa radio inakabiliwa na changamoto kubwa zinazotokana na vyombo vya habari vya teknolojia mpya, bado ina mustakabali mzuri. Radio bado ina nafasi kubwa katika nchi zinazoendelea, huku ikivumbua mbinu mpya na kuwa na wasikilizaji wa kudumu katika nchi zilizoendelea.”